Thursday, December 6, 2018

MAKAMU MWENYEKITI BARA MZEE MANGULA AZIFAFANULIA JUMUIA KIFUNGU KWA KIFUNGU MSTARI KWA MSTARI KTK KUFUNGA MAFUNZO YA KIMKAKATI KWA JUMUIA ZA CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Philipo Mangula  amefunga Mafunzo ya Kimkakati kwa Watendaji Makatibu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani

Akizungumza wakati akifunga Mafunzo hayo Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg Philipo Mangula amewataka viongozi hao kuyafanyia kazi yale yote waliojifunza katika mafunzo hayo ili kuendelea kukisaidia Chama kutimiza majukumu yake.

Pia Ndg Mangula alitumia nafasi hiyo kuwaonya watu wanaoibuka na kutaka kukwamisha kazi anazozifanya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa hawataweza.

“Niwatoe hofu viongozi wote kuwa nchi iko salama, zaidi tumuunge mkono Rais wetu kuwafichua watu wanaoiba mali za nchi,na tusiwanyamazie wale wote wenye nia ovu ya kutaka kikwamisha juhudi na kasi ya utendaji ya Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu ” alisema.

Aidha ndg Mangula amewapongeza Viongozi wote wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kwa kuandaa na kuyasimamia mafunzo hayo kwa watendaji wote wa ngazi za mikoa.

*#KulindanaKujengaUjamaa*
*#Tukutanekazini*

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa

No comments:

Post a Comment