Thursday, December 6, 2018

RC DODOMA MAVUNDE NI CHOMBO TUKITUMIE

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amemshukuru mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ndg Anthony Peter Mavunde kwa uchapakazi wake kwa wana Dodoma.

Pia amesema Mavunde ni chombo tukitumie, pia Dr Mahenge hakusita kuitumia hadhara hii kumshukuru Rais Magufuli kwa utekelezaji wa miradi iliyodumu ktk maandishi kwa miaka nenda rudi.

Leo hii imetimia kwa vitendo, asante sana Rais Magufuli asanteni wasaidi wenzangu wa Rais.

Pia nawashukuru na kuwapongeza viongozi wa jiji la Dodoma wanafanya kazi nzuri, wabunge wa Mkoa wa Dodoma na wana Dodoma wote asanteni sana.

Niwaase kulitumia hili gari alilotupa mbunge kwa makusudio yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment