Saturday, February 23, 2019

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA NDG MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA, WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick L. Mpogolo amewataka viongozi wa Mkoa wa Dodoma na wana CCM kwa ujumla kushiriki katika vikao vya mashina na kuimarisha mashina wanayotokana nao ili kukiongezea mtaji Chama cha Mapinduzi.

Ndg Mpogolo ameyasema hayo leo Wilaya ya Dodoma Mjini wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa CCM Kiwilaya kwa kuagiza viongozi wote bila kujali nafasi zao kushiriki katika vikao vya mashina na kuwatambua mabalozi wao na kuwapa ushirikiano unaostahili kwa ustawi wa Chama.

Akiwa katika ziara katika kiwanda cha mvinyo cha CETAWICO ,Ndg Mpogolo alipokea salamu za pongezi kutoka kwa wakulima wa zabibu ambao wamempongeza Mh Rais Dr Magufuli kwa kusimamia ushushaji wa tozo wa mchuzi wa zabibu kutoka Tsh 3,315 mpaka Tsh 450 kwa lita hali itakayopelekea kupatikana kwa soko la uhakika la zabibu zao. Wadau hao wa zabibu pia walitumia fursa hiyo kumshukuru Mh Anthony Mavunde Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini kwa namna alivyoisimamia hoja ya tozo ya mchuzi wa zabibu.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma mjini ndg Robert Daniel Mwinje amemuhakikishia ndg Mpogolo kwamba Dodoma itaendelea kuwa ngome ya CCM daima hasa kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero na changamoto za wananchi.

Aidha katika maadhimisho hayo ndg Mpogolo alipata nafasi ya kutembelea na kutoa msaada wa vyakula katika kituo maalum cha wanafunzi wenye mahitaji maalum Hombolo pamoja pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vipuri vya viwanda katika eneo la Hombolo.

1 comment:

  1. 1xBet Korean betting explained - Legalbet.co.kr
    1xBet Korean betting explained. If you're looking for a suitable betting exchange or site to bet 1xbet nigeria online with the most attractive odds, you are in the right place.

    ReplyDelete