Thursday, November 29, 2018

UVCCM DODOMA MJINI YAWAPONGEZA WANAZUONI NA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE.

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Dodoma mjini Ndg Said Jumanne Kasote, anatoa pongezi kubwa kwa wahitimu wote waliofanikiwa kumaliza masomo yao na kutunukiwa ngazi mbalimbali za kielimu kuanzia ngazi ya sekondari na vyuo vilivyomo Wilayani Dodoma mjini na nje ya Dodoma mjini, haswaa vijana wale wanaotaraji kuwa au wakazi wa Dodoma mjini.

Pia amependa kuwaasa wahitimu haswa katika vyuo mbalimbali juu ya suala la uzalendo na kuepuka fikra za kuajiriwa na serikali pindi wamalizapo masomo yao kwakuwa nafasi zinazotolewa na serikali ni chache kuliko idadi ya wanazuoni/wanafunzi wanaomaliza elimu zao kila mwaka, hivyo wasitegemee kuajiriwa na serikali tu. Zaidi kwa kutumia elimu waliyonayo waongeze juhudi za kujiajiri na pia kutambua thamani ya kujitolea kwenye kazi mbalimbali za kijamii kitu ambacho kitawanyanyua baadae

Amewaasa wajijenge ktk utamaduni wa kujiajiri ktk sekta mbalimbali hususan fursa ya kilimo ufugaji na fursa nyingine rafiki.

Pia mwenyekiti anawashauri wahitimu hao kuwa sehemu ya kutatu changamoto mbalimbali walizoziacha nyuma vyuoni kwa kutumia elimu zao na fursa mbalimbali.
Pia mwenyekiti amewakaribisha  vijana wote wenye mawazo chanya ya kimaendeleo wayawasilishe ofisi ya umoja wa vijana Wilaya ya Dodoma mjini nayo yatafanyiwa kazi.

Mwenyekiti pia anawapa moyo wale vijana waliopo vyuoni kukazana katika masomo na ambao hawajapata fursa hiyo kuendelea kupambana na inapopatikana fursa ya elimu basi wasisite kuingia katika mfumo huo. Zaidi amesisitiza umoja na mshikamano kwa maendeleo ya Dodoma mjini

Mwisho amewakaribisha wanazuoni na kuwaasa ndani na nje ya Dodoma watumike kwa maendeleo na maslai mapana kwa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment