*VIONGOZI WA DINI WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAZI NZURI,WACHANGIA UJENZI WA HOSPITAL YA UHURU DODOMA*
Viongozi wa Dini wa makanisa ya kipentekoste nchini**(CPCT)** wamempongeza *Mh Rais Dr John Pombe Magufuli* na serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuwahudumia watanzania na hasa wanyonge.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa *CPCT* *Askofu Dr.Yohana Masinga* katika ufunguzi wa Mkutano wa Injili-**Dodoma Miracle Festival** ambapo amewataka watanzania Kumuombea Rais Magufuli na Serikali kwa ujumla ili iendelee kufanya kazi nzuri ya kuwahudumia watanzania katika kuwaletea maendeleo.Katika kuunga mkono jitihada za Rais katika Ujenzi wa Hospital ya Uhuru Dodoma viongozi hao wa Dini wamechangia *Tsh 4,500,000*.
Akifungua Mkutano huo wa Injili Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde* amewapongeza viongozi wa dini kwa mchango wao mkubwa katika kudumisha **AMANI,UMOJA,MSHIKAMANO na UPENDO **miongoni mwa watanzania na kuwataka kuendelea kuiombea nchi yetu na viongozi wake ili Taifa Tanzania liendelee kustawi na kushamiri zaidi.
No comments:
Post a Comment