Friday, December 21, 2018

PINDA MGENI RASMI BARAZA UVCCM MKOA DODOMA

Kesho tarehe 22/12/2018 umoja wa vijana Mkoa wa Dodoma wanakusidia kufanya baraza la UVCCM Mkoa wa Dodoma ktk ukumbi wa CCM Mkoa wa Dodoma kuanzia saa mbili asubuhi.

Amesema mwenyekiti wake wa Mkoa ndg Billy Chidabwa kuwa taratibu zote zimeshakamilika na wajumbe wameshaanza kuwasili mjini Dodoma kwa ajili ya baraza hilo.

Pia mgeni rasmi ktk baraza hili ni waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati kuu Taifa ndg Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Hivyo natumia nafasi hii kuwakaribisha sana Dodoma mjini, wajumbe na wageni wote waalikwa.

No comments:

Post a Comment