Leo mwenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma ndg Msunga leo amezungumza na umoja wa wafanyabiashara soko kuu majengo na kupokea kero mbalimbali za wafanyabiashara na kuwaahidi kuzifikisha ktk vikao husika na kuwaahidi kuzisimamia mpaka zitatuliwe.
Kwakuwa kazi kuu ya CCM ni kuhakikisha wananchi wote wanaishi vizuri ktk maeneo yao ya biashara.
Pia ndg Msunga amemuagiza diwani wa kata ya Majengo ndg Msinta Mayaoyao kama pesa za ukarabati unaokusudiwa zipo basi zitolewe sasa.
Nao viongozi wa wafanya biashara wamemshukuru mgeni rasmi ndg Msunga pia wameomba awafikishie salamu zao za shukrani kwa mbunge wa Dodoma mjini kwa mengi aliyokwishawafanyia na anayoendelea kuwafanyia wafanyabiashara wa soko kuu.
Nae ndg Msunga amewaahidi viongozi hao kufikisha salamu za mbunge isipokuwa amewaasa kushirikiana na kuheshimiana baina yao wao kwa wao kwa kufata taratibu za kiuongozi pindi mnapohitaji kuondoa tofauti zenu
No comments:
Post a Comment