Thursday, March 14, 2019

WACHIMBAJI WADOGO NAMUNGO AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA MADINI

Tarehe 13/03/2019

Wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu katika eneo la Namungo,Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi wamempongeza na kumshukuru Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kusikiliza na kutatua changamoto kubwa zilikuwa zinaikabili sekta ya madini hasa kodi ya zuio (withholding Tax) ambayo imefutwa kufuatia marekebisho ya Sheria yaliyowasilishwa Bungeni katika mkutano wa bunge lililopita, pia wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa Majaliwa kwa utekelezaji wa ahadi za kujenga Daraja na usambazaji wa umeme katika eneo la Namungo ambalo hivi sasa kuna umeme wa kutosha kuendesha migodi.

Shukrani hizo zimetolewa leo na Ndg Suleiman Chimbwalu, kwa niaba ya wachimbaji wote,kwenye machimbo ya Dhahabu eneo la Namungo Wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ambaye pia ametumia fursa hiyo kuelezea mpango wa Serikali katika kuwawezesha kundi hili kubwa la Vijana ili kutengeneza nafasi nyingi zaidi za Ajira kwa kuwataka wachimbaji kukaa katika vikundi ili wapatiwe mkopo wa kununua vifaa vya uchimbaji na mashine za kusaga mawe ili kuongeza tija.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Mavunde ametembelea katika kata ya  Mnacho,Kijiji cha Chimbila “A” katika Bonde la Nachikalala kukagua ujenzi wa Kitalu Nyumba kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga katika mradi wa kuwajengea uwezo Vijana ambapo inatarajiwa kuwa Vijana 18,400 nchi nzima watanufaika na mpango huu wa kuwajengea ujuzi kupitia mafunzo ya kilimo kupitia Kitalu Nyumba na utengenezwaji wa Kitalu Nyumba

Wednesday, March 6, 2019

MBUNGE MAVUNDE AWATAKA WANAWAKE DODOMA MJINI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

Tarehe 07/03/2019

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewataka wanawake wa Dodoma Mjini kuchangamkia fursa za kiuchumi na kutokubali kukatishwa tamaa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi ili kujijengea heshima kubwa katika jamii.

Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika kongamano lilioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kitengo cha wanawake katika shule ya sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku ya MWANAMKE DUNIANI.

“Natamani kuwaona wanawake wa Dodoma mkiwa mbele kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujijengea nguvu ya kiuchumi na kujiongezea kipato.

Dodoma hivi sasa baada ya tamko la Makao Makuu fursa nyingi sana zimejitokeza hivyo msilaze damu kwa kubaki kuwa waangaliaji na badala yake na ninyi mshiriki moja kwa moja”Alisema Mavunde

Akisoma Risala kwa niaba ya walimu hao kitengo “KE” *Mwl Joyce Kaishozi* ameeleza kwamba Chama hicho kimejipanga vyema kumjengea uwezo mwalimu mwanamke ili jamii kutambua nafasi ya Mwalimu mwanamke na ndio maana katika kongamano walimu wamepata nafasi kupata mafunzo katika maeneo ya AFYA UJASIRIAMALI  na UONGOZI BORA.

Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Mjumbe Wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Ndg Leila Burhan Ngozi na Mbunge wa Viti Maalum-Dodoma Mh Felister Bura

NAIBU WAZIRI MAVUNDE ATOA RAI KWA SEKTA BINAFSI KUWAJENGEA UJUZI VIJANA WA TANZANIA NA KUWAAJIRI

Tarehe 06/03/2019

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ametoa rai kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuwajengea ujuzi vijana wa Tanzania kupitia program mbalimbali za kukuza ujuzi ili kuwajengea uwezo na sifa za kuajirika ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa jana na Mh Mavunde katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi tuzo kwa washindi wa shindano la andiko la mradi lililofadhiliwa na kampuni ya TOTAL, ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza kampuni ya TOTAL kwa kuwawezesha vijana kuongeza mtaji na pia kwa kusaini makubaliano na chuo kikuu Dar es salaam(UDSM) kuchukua wanachuo 20 kwa ajili ya kuwapatia mafunzo na kuwapatia uzoefu katika fani mbalimbali.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, mkurugenzi mtendaji wa TOTAL Tanzania  ndg Tarik Moudaffal amesema kwamba kila mwaka kampuni yake hushindanisha vijana wenye andiko la mradi ambapo huwawezesha kiasi cha fedha kwa ajili ya kutekeleza wazo hilo la biashara ikiwa ni pamoja na kuwalea kupitia viatamizi(Incubator) nchini Ufaransa kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi.

Katika Shindano la Total Startupper of the year 2019 mshindi ni Bi Doreen Noni ambaye amewapiku vijana wengine 15 na kuzawadiwa kiasi cha Tsh's 30,000,000.

Friday, March 1, 2019

MBUNGE MAVUNDE ATIMIZA AHADI YA UTATUZI WA KERO YA MAJI SHULE YA SEKONDARI MPUNGUZI.

Tarehe 01/03/2019
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo ametimiza ahadi yake ya kutatua kero ya Maji katika Shule ya Sekondari Mpunguzi Dodoma kwa kuzindua mradi wa maji ambao utahakikisha upatikanaji wa Maji safi na Salama shuleni hapo.

Mavunde alitoa ahadi hiyo ya kutatua kero hiyo wakati wa mahafali ya kidato cha IV mwaka 2018 na kuahidi kushirikiana na Jiji la Dodoma kwa kuchangia baadhi ya gharama na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu wa maji.

“Namshukuru ndg Godwin Kunambi mkurugenzi wa Jiji kupitia idara ya maji kwa namna ambavyo waliusimamia na kutekeleza mradi huu, kwa upande wangu nimewaletea tenki kubwa la lita 5000 kuhifadhi maji na mashine ya kuchuja Maji(Life straw) ili muweze kunywa maji safi na salama wakati wote,na kwasasa tumechimba visima viwili vya maji katika kata ya Mpunguzi ili kuhakikisha maji yanapatikana muda wote na kwa uhakika”Alisema Mavunde

Akisoma taarifa ya awali,Makamu Mkuu wa Shule ya Mpunguzi Sekondari Mwl Abdallah Mshamu amesema Shule hiyo imekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji tangu mwaka 2005 na hivyo kulazimu wanafunzi kutafuta maji nje ya eneo la shule jambo ambalo lilikuwa linapotwza muda mwinginwa wanafunzi hao kujisomea lakini pia kuhatarisha usalama wao hasa kwa kuvuka barabara kuu ya Iringa kufuata maji upande wa pili wa shule.

Wakati huo huo,Mh Mavunde ameahidi kukarabati ofisi ya Walimu na kununua viti 30 vya walimu, kuwafungia wanafunzi TV kubwa katika bwalo lao na mwishoni amegawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tshs 1,800,000/= kwa timu 8 zitakazoshiriki katika Kombe la Mavunde Cup kata ya Mpunguzi itakayojumuisha pia Timu ya Shule ya Sekondari Mpunguzi.

Wednesday, February 27, 2019

SEKTA BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI JUU YA MAFUNZO YA KUWAANDAA WATANZANIA KUSHIKA NYADHIFA ZA JUU ZA UONGOZI KTK MAKAMPUNI(CEOrt)

Tarehe 26/02/209
Jukwaa La Taasisi ya  Wakurugenzi na wamiliki wa makampuni binafsi Tanzania**(CEOrt)** kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira limekuja na mpango maalum wa kuwawezesha watanzania kushika nyadhifa za juu za Uafisa Mtendaji Mkuu**(CEOs)** na Ukurugenzi Mtendaji**(MDs)** katika Makampuni na Taasisi mbalimbali kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo yatakayoratibiwa na Chuo cha Strathmore Business School** (SBS)**.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CEOrt *Ndg Sanjay Rughani* wakati akijadiliana mpango huo na Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde **katika kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata mafunzo ili kushika nyadhifa za juu katika Makampuni hasa kutokana na kuonekana kwamba kuna upungufu mkubwa wa watu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo kwa sasa ambapo kwa kuanzia juu ya Watanzania* *20* wataanza kujengewa uwezo kwa mwaka huu na kuendelea kila mwaka kuongeza idadi.

Akizungumza katika kikao hicho,Naibu Waziri Mavunde ameishukuru Taasisi ya *CEOrt* kwa kuja na mpango wenye tija wa kuijengea uwezo nguvu kazi ya Watanzania ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushika nyadhifa za juu katika makampuni na Taasisi na kuahidi,kwa niaba ya Serikali, kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa Programu hii yenye tija kwa maslahi ya nguvu kazi ya Tanzania.

“Hili jambo ni la kizalendo, tunaliunga mkono kama Serikali.Na sisi kupitia Mpango wa Ukuzaji Ujuzi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tunatekeleza mafunzo ya vitendo *(Apprenticeship)* wahitimu wa Vyuo vikuu na Vyuo vya Elimu ya Juu ili kuwajengea uwezo na kuwa na sifa za kuajirika”Alisema Mavunde

Monday, February 25, 2019

NAIBU KATIBU MKUU WAZAZI BARA NDG TIJA MAGOMA AHIMIZA UMOJA NA UPENDO KWA VIONGOZI NA WANACHAMA DODOMA PIA KUSHUKUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA

Naibu Katibu Mkuu wa wazazi Bara Ndg Tija Magoma amewataka viongozi wa CCM Dodoma mjini na wana CCM kwa ujumla kushiriki katika vikao vya mashina na kuimarisha umoja na mshikamano ili kukiongezea mtaji na upendo Chama Cha Mapinduzi.

Ndg Magoma ameyasema hayo leo Dodoma wakati wa maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa CCM kwa kuagiza viongozi wote bila kujali nafasi zao kushiriki katika vikao vya mashina na kuzidisha umoja na upendo kwa jamii tunayoiongoza.

Akiwa katika ziara pia alitembelea watoto wanaoishi ktk kijiji cha matumaini Dodoma mjini.

Akifungua mkutano huo mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Dodoma ndg Amanuel Mkumbo.
Amemuhakikishia naibu katibu mkuu kuwa wa Dodoma kupo shwari na salama kwa CCM na wote wanaoendelea kuingia Dodoma licha ya changamoto ndogondogo za kibinaadamu zinazozuilika na kutatulika.

Saturday, February 23, 2019

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA NDG MPOGOLO AWATAKA VIONGOZI MKOANI DODOMA KUSHUKA CHINI KUIMARISHA MASHINA, WAKULIMA WA ZABIBU WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick L. Mpogolo amewataka viongozi wa Mkoa wa Dodoma na wana CCM kwa ujumla kushiriki katika vikao vya mashina na kuimarisha mashina wanayotokana nao ili kukiongezea mtaji Chama cha Mapinduzi.

Ndg Mpogolo ameyasema hayo leo Wilaya ya Dodoma Mjini wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa CCM Kiwilaya kwa kuagiza viongozi wote bila kujali nafasi zao kushiriki katika vikao vya mashina na kuwatambua mabalozi wao na kuwapa ushirikiano unaostahili kwa ustawi wa Chama.

Akiwa katika ziara katika kiwanda cha mvinyo cha CETAWICO ,Ndg Mpogolo alipokea salamu za pongezi kutoka kwa wakulima wa zabibu ambao wamempongeza Mh Rais Dr Magufuli kwa kusimamia ushushaji wa tozo wa mchuzi wa zabibu kutoka Tsh 3,315 mpaka Tsh 450 kwa lita hali itakayopelekea kupatikana kwa soko la uhakika la zabibu zao. Wadau hao wa zabibu pia walitumia fursa hiyo kumshukuru Mh Anthony Mavunde Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini kwa namna alivyoisimamia hoja ya tozo ya mchuzi wa zabibu.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma mjini ndg Robert Daniel Mwinje amemuhakikishia ndg Mpogolo kwamba Dodoma itaendelea kuwa ngome ya CCM daima hasa kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero na changamoto za wananchi.

Aidha katika maadhimisho hayo ndg Mpogolo alipata nafasi ya kutembelea na kutoa msaada wa vyakula katika kituo maalum cha wanafunzi wenye mahitaji maalum Hombolo pamoja pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vipuri vya viwanda katika eneo la Hombolo.