Tarehe 01/03/2019
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo ametimiza ahadi yake ya kutatua kero ya Maji katika Shule ya Sekondari Mpunguzi Dodoma kwa kuzindua mradi wa maji ambao utahakikisha upatikanaji wa Maji safi na Salama shuleni hapo.
Mavunde alitoa ahadi hiyo ya kutatua kero hiyo wakati wa mahafali ya kidato cha IV mwaka 2018 na kuahidi kushirikiana na Jiji la Dodoma kwa kuchangia baadhi ya gharama na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu wa maji.
“Namshukuru ndg Godwin Kunambi mkurugenzi wa Jiji kupitia idara ya maji kwa namna ambavyo waliusimamia na kutekeleza mradi huu, kwa upande wangu nimewaletea tenki kubwa la lita 5000 kuhifadhi maji na mashine ya kuchuja Maji(Life straw) ili muweze kunywa maji safi na salama wakati wote,na kwasasa tumechimba visima viwili vya maji katika kata ya Mpunguzi ili kuhakikisha maji yanapatikana muda wote na kwa uhakika”Alisema Mavunde
Akisoma taarifa ya awali,Makamu Mkuu wa Shule ya Mpunguzi Sekondari Mwl Abdallah Mshamu amesema Shule hiyo imekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji tangu mwaka 2005 na hivyo kulazimu wanafunzi kutafuta maji nje ya eneo la shule jambo ambalo lilikuwa linapotwza muda mwinginwa wanafunzi hao kujisomea lakini pia kuhatarisha usalama wao hasa kwa kuvuka barabara kuu ya Iringa kufuata maji upande wa pili wa shule.
Wakati huo huo,Mh Mavunde ameahidi kukarabati ofisi ya Walimu na kununua viti 30 vya walimu, kuwafungia wanafunzi TV kubwa katika bwalo lao na mwishoni amegawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tshs 1,800,000/= kwa timu 8 zitakazoshiriki katika Kombe la Mavunde Cup kata ya Mpunguzi itakayojumuisha pia Timu ya Shule ya Sekondari Mpunguzi.
No comments:
Post a Comment