Sunday, December 30, 2018

KIKOMBO RANGER'S YANYAKUA MAVUNDE CUP

Fainali za Mavunde Cup kata ya Kikombo zimekamilika leo kwa Timu ya Kikombo Rangers kuitandika Timu ya Jamhuri ya Chololo kwa bao moja bila na hivyo kutawazwa mabingwa na kuzawadiwa Tsh 500,000 seti ya jezi na mipira miwili.

Akihutubia wananchi katika fainali hizo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* amewataka Vijana kujiendeleza katika michezo na kuwahamasisha kuzigeuza timu zao kuwa vikundi vya Uzalishaji mali ili kunufaika na mikopo ya maendeleo ya Vijana.

No comments:

Post a Comment