24 Dec 2018
Na Mwl Raymond Mangwala
Ndugu wanahabari,
Leo tarehe 24/12/2018 *Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi* tumewaita hapa kuzungumzia Utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano(5) inayoongozwa na *Rais Dkt John Pombe Magufuli* katika kipindi cha miaka mitatu.
Mpaka sasa Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Dkt Magufuli imefanya utekelezaji mkubwa wa mambo mbalimbali ya maendeleo yanayogusa moja kwa moja maslahi mapana ya wananchi ambayo yameainishwa katika Ilani ya CCM 2015-2020.
Ndugu Wanahabari,
Yafuatayo ni mambo mbalimbali ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli;
1. *Ujenzi wa Reli ya Kisasa(Standard Gauge)*.
Tumeona Rais akifanya uzinduzi wa ujenzi huu wa reli ya kisasa ambayo itatumia umeme kuanzia Dar es salaam mpka Morogoro, ambapo ikikamilika inatarajiwa kuwa na Spidi ya kilomita 160 kwa saa.Lakini pia kwa ujenzi huu tutapata urahisi wa usafiri wa abiria na mizigo, pia inatarajia kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi jirani kama vile Rwanda,DRC , Burundi kwa kuwa baadaye itakwenda hadi nchi zote zilizoko mpakani mwa Tanzania.Jambo kubwa zaidi mradi huu utatoa Ajira kwa Vijana.
2. *Ujenzi wa Flyover ya Tazara kwa Mfugale*.
Ujenzi wa barabara ya juu Tazara katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela ambao umekamilika kwa sehemu kubwa umepunguza adha ya foleni kwa wakazi wa Dar es salaam. Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 99.50. Daraja hilo limeboresha mifumo ya miundombinu ya usafiri na kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara hizi.
3. *Ujenzi wa Daraja la Selander*
Daraja hili litakuwa na njia nne za magari, sehemu ya watembea kwa miguu na litadumu kwa zaidi ya miaka 100.Kwa maelezo ya kitaalamu Daraja hili linauwezo wa kubeba tani 180 kwa wakati mmoja.Pamoja na barabara unganishi litakuwa na urefu wa kilomita 6.23.Gharama za ujenzi wa Daraja hili Dola za kimarekani Milioni 112.8 ambapo nchi ya Korea itatoa Dola Milioni 91.03 na Tanzania itatoa dola milioni 21,822.
4. *Ujenzi wa Barabara ya Njia Nane kutoka Kimara-Kibaha*.
Tumesikia Barabara hii ya Kimara mpaka Kibaha itakuwa na urefu wa kilomita 19.2 .Ujenzi ulishaanza toka Julai mwaka huu. Barabara hii kwa siku itatarajiwa kupitisha Magari elfu 50 na Barabara hii ya njia nane inanjengwa na Mkandarasi mzawa ikikamilika itaitwa ‘TANZANIA ONE’.Kumbuka fedha zote za ujenzi wa mradi huu zinatolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30.
5. *Mradi wa Umeme Mto Rufiji(Stiegler’s Gorge Hydropower Dam)*.
Mradi huu ni mradi wa kihistoria katika nchi yetu na lengo ni kuwa kichocheo katika Uchumi wa Viwanda.Bwawa hili la kufua umeme katika mto Rufiji ni bwawa la sitini(60) kwa ukubwa na miongoni mwa mabwawa 70 Duniani ambapo Afrika ni bwawa la nne na Afrika mashariki ni bwawa la kwanza.Umeme wa mradi huu utatumika kuendesha mitambo ya Treni ya kisasa ya Standard Gauge na pia kusambazwa Vijijini.Mradi huu ukikamilika unataweza kuzalisha umeme wa Megawatts 2115 hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya Uchumi.Itakumbukwa gharama za uendeshaji huu wa Stiegler’s Gorge zipo chini ambapo Megawatt 1= Shilingi 10 wakati Miradi mingine Megawatt 1 ni shilingi 35.
6. *Elimu Bure*.
Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi imeendelea kushughulika na shida za watu kwa kuleta Elimu Bure.Serikali inatoa shilingi Bilioni 22.2 kwa kila mwezi ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari.Tangua kuanzishwa kwa Elimu bure uandikishwaji wa watoto wa awali na darasa la kwanza umeongezeka, pia ufaulu wa mitihani umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 70 mwaka 2016 hadi wastani wa asilimia 78 mwaka 2018.
7. *Ununuzi wa Korosho*.
Itakumbukwa mnamo tarehe 12 Novemba 2018 Rais Dkt John Pombe Magufuli alitoa maamuzi ya Serikali juu ya kununuzi Korosho, ambapo alisema korosho itanunuliwa kwa shilingi 3300/= kwa kilo moja na ni korosho isiyobanguliwa.
Kwa maagizo haya ameonyesha kumjali mkulima wa Tanzania.
8. *Ununuzi wa Ndege mpya*.
Jana Tanzania kwa mara ya kwanza tumeshuhudia tukileta ndege yetu aina ya Airbus A 220-300 iliyopewa jina la Dodoma ambapo kwa bara la Afrika ndio nchi ya kwanza kununua.Idadi ya abiria wanaotumia shirika la ndege ATCL imeongezeka kutoka 5600 hadi kufika abiria elfu 34,000 kwa mwezi.Hii ni Ndege ya tano kuwasili nchini toka katika kipindi cha miaka 3 ya Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli na wakati huo huo mwezi Januari tunategemea kupokea Ndege kama hii ya Airbus A220-300 itakayoitwa Ngorongoro.
Ndugu Wanahabari,
Kutoka na mambo hayo makubwa ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli, Umoja wa Vijana wa CCM Unaoongozwa na Mwenyekiti Ndugu Kheri Denice James Tunapongeza Serikali ya Awamu ya Tano na kuendelea kuwatia Moyo Rais na Watendaji wake ili kuendelea kushughulika na kero za watu ambapo tunategemea kwayo ifikapo 2020 Ilani ya CCM itakuwa imetekelezwa kwa asilia 100%.
Viva Vijana Vivaaa!
KIDUMU CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment