Leo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa udiwani kata ya Dodoma Makulu ndg Petronila Kagumu na Aneth Mnana wamemtangaza ndg Paschal Matulaa kuwa diwani mteule baada ya kupita bila kupingwa.
Wamesema mpaka muda wa kurudisha fomu kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi unaisha ni ndg Paschal Matulaa pekee ndiye aliyerejesha fomu yake ya uchaguzi.
Hivyo kwa mamlaka waliyopewa na serikali wanamtangaza ndg Paschal Matulaa kuwa diwani mteule wa kata ya Dodoma Makulu.
Pia zoezi hili la urudishaji wa fomu ulienda sanjari na uchangiaji damu salama.
Nae Dr Leyla ambae ndio msimamizi mkuu wa kitengo cha damu salama Mkoa wa Dodoma amewashukuru wananchi kwa uchangiaji huu pia hakusita kumshukuru diwani mteule kwani yeye ndiye chachu ya uchangiaji huu wa leo.
No comments:
Post a Comment