Saturday, February 23, 2019

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWASHUKIA WAAJIRI WANAOKWEPA KODI KWA KUDANGANYA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewashukia waajiri wote wanaotoa taarifa ambazo si sahihi za mishahara ya wafanyakazi kwa lengo la kukwepa kodi na pia kuchangia mchango mdogo katika mifuko ya hifadhi ya jamii tofauti na mshahara wake.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziti Mkuu Mh Anthony Mavunde wakati akiongea na waandishi wa habari katika Jiji la Mbeya na kubainisha kwamba Ofisi ya kamishna wa kazi inaendelea na ukaguzi wa kawaida ili kuwabaini waajiri hao na kuwachukulia hatua za kisheria.

“Tutafanya ukaguzi maalum ili kuwabaini waajiri ambao kwenye payroll yao wanaainisha mshahara pungufu wa mfanyakazi na kumlipa mfanyakazi kiasi kilichobakia kwa utaratibu ambao ni nje ya mfumo wa kawaida wa kumbukumbu hali inayoikosesha Serikali mapato kupitia kodi,lakini pia kuwasilisha mchango mdogo katika mifuko ya hifadhi ya Jyamii ambapo mwisho wa siku hupelekea mafao kidogo ya mfanyakazi tofauti na mshahara wake. Nawataka wafanyakazi wote nchi nzima kutoa taarifa hizi ili kuwabaini waajiri hawa na kuchukuliwa hatua za kisheria”Alisema Mavunde

No comments:

Post a Comment