Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira katika utekelezaji wa programu ya (RPL) imedhamiria, katika awamu ya kwanza, kuwafikia na kurasimisha ujuzi kwa takribani Watanzania 10,000 kwa mwaka 2019/2020.
Hayo yamesemwa leo katika ukumbi wa Royal Tughimbe Jijini Mbeya na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde wakati akifungua kongamano la mafundi wa Mkoani Mbeya,ambapo alibainisha kwamba Serikali inatekekeleza programu ya kurasimisha ujuzi kwa watu wenye ujuzi lakini ambao hawajapitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya Ufundi kwa kuwapatia vyeti vya ufundi pasipo wao kusoma chuo cha ufundi hasa baada ya kuwa wamepitishwa na wakufunzi na wataalamu kutoka VETA.
“Lengo letu kama serikali ni kuwajengea uwezo na ujuzi watanzania wengi zaidi ili washiriki kama nguvu kazi katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa Reli(SGR) mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda-Tanga,Mradi wa kufua umeme wa Stiegler’s Gorge na miradi mingine mikubwa nchini”Alisema Mavunde.
Akiwasilisha taarifa fupi, mkurugenzi wa Kampuni ya Fundi Smart ndg Freddy Herbert Pole amesema lengo la kukusanya mafundi wao ni kuwajengea uelewa kwa kuwapa elimu ya masuala ya fedha, afya na sheria na kuwatengenezea mfumo mzuri wa ufanya kazi zao za kila siku kwa kuzingatia weledi, taratibu na sheria.
No comments:
Post a Comment