Katika kuitikia wito wa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli wa kuwataka viongozi kushuka chini na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi, jumla ya mawaziri na manaibu waziri 9 wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikuwa katika ukumbi wa AICC jijini Arusha kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha na baadaye kuzipatia ufumbuzi kero hizo.
Akiwasilisha taarifa fupi ya ufunguzi,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Mashaka Gambo alibainisha kwamba ameandaa mkutano huo wa pamoja ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kero za mara kwa mara zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara Mkoani Arusha ili kupitia ufumbuzi wa kero hizo ziboreshe mazingira ya ufanyaji biashara na kukuza sekta ya utalii ili kuongeza mapato ya nchi.
Wakijibu kero mawaziri na manaibu waziri kwa pamoja wamewahakikishia wawekezaji hao kwamba ni dhamira ya serikali kuhakikisha inaweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara na kuondoa vikwazo vitakavyoaathiri ukuaji wa sekta mbalimbali za kiuchumi.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri Mh Dr Philip I. Mpango, Mh Angela Kairuki, Mh Isack Kamwelwe, Mh Kangi Lugola, Mh January Makamba, Mh George Kakunda na Manaibu Waziri Mh Constantine Kanyasu, Abdallah Ulega na Mh Anthony Peter Mavunde.
No comments:
Post a Comment