Leo tarehe 14/02/2019
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ndg Anthony Mavunde leo amewatembelea wakina mama wajawazito katika vituo vya afya na zahanati Jijini Dodoma na kutoa msaada wa mifuko ya Vifaa vya kujifungulia(Delivery Pack) pcs 350 yenye thamani ya Tsh's 7m ,mashuka pcs 100 yenye thamani ya Tsh's 1.1m ,pakiti pcs 40 za dawa aina ya dinoprostone zenye thamani ya Tsh's 1m na cartons 30 za maji ya kunywa, hali iliyopelekea furaha kubwa kwa wakina mama wajawazito na kushindwa kuficha hisia zao na kudondosha machozi ya furaha.
Nimeamua kuitumia siku ya leo kuonesha upendo kwa wakina mama wangu wa Dodoma kwa kusaidia vifaa hivi muhimu wakati wa kujifungua, hii ni shukrani nairudisha kwenu kwa upendo wenu mkubwa kwangu ”alisema mbunge Mavunde.
Akimshukuru mbunge Mavunde kwa msaada huo mkubwa, mganga mkuu wa Jiji la Dodoma Dr Gatete Mahava
amemuomba mbunge Mavunde kuendelea kusaidiana na serikali kutatua changamoto katika sekta ya afya hasa katika kituo cha afya cha Makole ambacho kimefanyiwa upanuzi mkubwa baada ya kukamilika ujenzi wa wodi ya wakina mama kupitia fedha kiasi cha Tsh's 500m zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afya.
Katika tukio hilo Mavunde aliambatana na viongozi wa CCM Wilaya ya Dodoma mjini ,Mbunge wa viti maalum ndg Esther Bura, madiwani wa kata, wasanii na mama lishe wa soko kuu Majengo.
No comments:
Post a Comment