Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM na mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndg Leylah Ngozi leo tarehe 10 Februari, 2019 ameendelea na ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Dodoma
Leo alikuwa ktk Wilaya ya Dodoma mjini ktk tarafa ya Kikombo.
Ndg Leylah Ngozi amekagua uhai wa Chama Cha Mapinduzi ktk tarafa ya Kikombo na kuzungumza na viongozi wa chama kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata na Wilaya lengo ni kukumbushana namna bora ya kushiriki vyema na kukipatia Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo ifikapo kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020 na kutokukubali kurudia makosa ya uchaguzi wa mwaka 2014 na 2015.
Katika kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Ndg Leylah Ngozi pia ameshiriki katika shughuli za kijamii kwa kufanya usafi ktk kituo cha afya ktk tarafa ya Kikombo Wilayani Dodoma.
Ndg. Ngozi amewataka wanachama wa CCM wa Mkoa wa Dodoma na hususan Wilaya ya Dodoma mjini na tarafa ya Kikombo kushikamana na kuwa wamoja katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi ktk tarafa ya Kikombo kinashinda kwa kishindo katika chaguzi zake zote zijazo za serikali za mitaa mwaka huu 2019 na uchaguzi mkuu mwakani 2020.
Amesema kama ambavyo serikali yetu ya awamu ya tano ilivyojipambanua kufanya kazi kwa vitendo na kujipambanua kikamilifu katika utekelezaji wa Ilani yake kwa uadilifu na umakini mkubwa ni wajibu kuwa na muendelezo wa kuitafsiri imani ya CCM kwa vitendo na ndio maana hata kaulimbiu yetu ya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM inatoa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Hivyo niwanasihi viongozi, wanachama na wakerekwetwa wa CCM tuendelee kuiunga mkono serikali yetu ya CCM pia tuendelee kumuunga mkono mwenyekiti wetu wa CCM Dr John Pombe Joseph Magufuli ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchapa kazi kwa bidii na uadilifu kama kauli mbiu yetu inavyosema
KAZI NDIO KIPIMO CHA UTU.
Mjumbe huyo wa kamati kuu na mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma aliwataka wana CCM na wananchi wote kupuuzia uzushi na uchochezi unaoenezwa dhidi ya wasioitakia mema Taifa letu. Napia alipata fursa yakuwaeleza umuhimu wa kuendelea kulinda mapinduzi matukufu ya Zanzibar, uhuru pamoja na muungano wetu.
Nchi yetu ni Nchi ya amani na ni miongoni mwa nchi yenye utajiri mkubwa wa asili Duniani hivyo ni dhahiri maadui hawawezi kukosekana wapo na wataendelea kuwepo watatafuta kila mbinu kutudhoofisha kwa maslahi yao,kwa sasa wameminywa kila kona na Mzalendo Magufuli hivyo wameamua kutafuta kila njia kumtikisha lakini wamegundua kuwa Rais Magufuli ni mwamba imara usiotikisika..Tuendelee kumuombea kheri Rais wetu tusisikilize kelele za mabwanyenye au mawakala wao.
Ndg. Ngozi aliwashukuru wana CCM na wananchi wote wa Wilaya ya Dodoma mjini na kata ya Kikombo kwa mapokezi makubwa na kujitoa kwao kujumuika katika muendelezo wa maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment