Saturday, February 9, 2019

KATIBU MKUU CCM DR BASHIRU ALLY KAKURWA AWAKABIDHI UVCCM NG'OMBE 20 WA KISASA.

Leo Tarehe 9-2-2019 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, (MCC) Komred Kheri Denice James  kwa niaba ya katibu mkuu wa CCM Amekabidhi mradi wa ng'ombe 20 kwa umoja wa vijana wa CCM wa mkoa wa Simiyu.

Akitoa hotuba fupi ya kukabidhi Ng'ombe hao kwa umoja wa vijana wa CCM mkoani Simiyu,Mwenyekiti UVCCM Taifa Komred Kheri Denice James (MCC)Amewasisitiza vijana kuwatunza vizuri Ng'ombe hao,na wawatumie kama mradi wa mfano kwa vijana kujifunza ufugaji wa kisasa na kuujengea msingi wa kuwa kitega uchumi kitacho isaidia jumuiya kujitegemea.              

*"Ndugu vijana wenzangu mifugo hii tuliopewa leo na  Katibu Mkuu wetu wa  CHAMA ni ishara ya imani kubwa alio nayo kwa jumuiya yetu na  ni ujumbe wa kuitaka jumuiya kujitegemea kiuchumi na kuwa mfano bora wa shughuli za uzalishaji katika kukuza uchumi wa taifa letu"*

Komred Kheri amemshukuru Katibu mkuu wa CCM kwa mchango huo mkubwa ktk jumuiya, na kuahidi kushirikiana na viongozi wenzake kuweka utaratibu bora wa kusimamia mradi huo ili uzae matunda yalio kusudiwa.Aidha Mwenyekiti amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Simiyu Komred Anthony Mtaka kwa kusaidia eneo  la ufugaji na kuwezesha shughuli mbalimbali za chama na jumuiya mkoani humo.        

Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya,Mkuu wa mkoa wa Simiyu pamoja na vijana wa CCM wilayani Bariadi.        

*#Tukutane kazini..*

No comments:

Post a Comment