Saturday, February 9, 2019

MBUNGE DITOPILE AUNGURUMA BUNGENI BAADA TOZO YA USHURU KUPUNGUZWA KUTOKA TSH'S 3,315/= MPAKA TSH'S 450/=

Hatimaye Serikali sikivu ya CCM chini ya uongozi wa *Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli* imesikia kilio cha wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma cha ukosefu wa soko la zabibu kutokana na tozo kubwa ya ushuru wa bidhaa iliyokuwa ikitozwa  Tsh 3,315 kwa lita kwa kinywaji kikali kitokanacho na mchuzi wa zabibu.

Akichangia leo Bungeni katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Na.2/2019 Mbunge wa Viti Maalum Mh Mariam Ditopile ameishukuru serikali kwa kuleta mabadiliko hayo ya ushuru wa bidhaa na kupunguza tozo hiyo ambayo itawasaidia wakulima kupata soko la uhakika wa zabibu zao.

Aidh Mh Ditopile amatumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa Bunge Mh Job Ndugai kwa kulisimamia suala hili kuelezea changamoto kubwa wanayoipata wakulima mkoani Dodoma,vile vile amempongeza Mh Anthony Mavunde Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye aliliwasilisha ombi hili pia kwa Mh Rais tarehe 23.04.2018 wakati wa ufunguzi wa Jengo la PSPF.

Kwa nyakati tofauti Mh Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kuzitaka Wizara husika kulifanyia kazi suala hili kwa manufaa ya wakulima wa zabibu wa mkoa wa Dodoma.

Hatimaye leo Bunge la Jamhuri ya Tanzania limepitishwa muswada wa marekebisho ya Sheria ambao umelenga,pamoja na mambo mengine,kupunguza tozo ya Vinywaji vikali vitokanavyo na mchuzi wa Zabibu.

No comments:

Post a Comment