MLEZI WA CCM MKOA WA DODOMA NDG LEYLA NGOZI (MCC) AMEWAASA WANA CCM WA MKOA WA DODOMA KUSHIKAMANA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU.
Mjumbe Wa Kamati Kuu Ya Halmashauri kuu Ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndg Leyla Ngozi jana Tarehe 05 Februari, 2019 ameanza ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Dodoma
Ikiwa ni siku ya kwanza ktk Wilaya ya Kondoa mjini na Vijijini Ndg Leyl Ngozi Amekagua uhai wa Chama na kuzungumza viongozi wa Chama kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya hadi Mkoa lengo ni kutoa semina ya namna bora ya kushiriki vyema na kukipatia Chama cha Mapinduzi ushindi wa kishindo ifikapo kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu.
Katika kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Ndg Leyla Ngozi pia ameshiriki katika shughuli za kijamii za ujenzi wa kituo cha afya kata ya Bereko Wilayani Kondoa akishirikiana na viongozi mbalimbali na wana CCM waliokuwepo katika sherehe hizo nakupanda miti katika eneo la kituo cha afya cha Bereko.
Aidha Ndg. Leyla Ngozi amewapokea wanachama wapya wanaotokana na vyama vya upinzani akiwemo mwenyekiti wa kata pamoja na katibu wake na wanachama mbalimbali wote ni katika chama cha CUF .
Ndg. Ngozi amewataka wanachama wa CCM wa Mkoa wa Dodoma na hasa Wilaya ya Kondoa kushikamana na kuwa wamoja katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo katika chaguzi zake zote zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
Kama ambavyo serikali yetu ya awamu ya tano ilivyojipambanua kufanya kazi kwa vitendo na kujipambanua kikamilifu katika utekelezaji wa Ilani kwa uadilifu na umakini mkubwa, wajibu huo ni muendelezo wa kuitafsiri imani ya CCM kwa matendo na ndio maana hata kaulimbiu yetu ya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM inatoa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Hivyo niwanasihi tuendelee kuiunga mkono serikali yetu ya CCM na pia kuendelea kumuunga mkono mwenyekiti wetu wa CCM Dr. John Pombe Magufuli ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukachapa kazi kwa bidii na uadilifu ."* Aliyasema hayo Ndg. Ngozi
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma aliwataka wana CCM na wananchi wote kupuuzia uzushi na uchochezi unaoenezwa dhidi ya wasioitakia mema Taifa letu.
Napia alipata fursa yakuwaeleza umuhimu wa kuendelea kulinda mapinduzi matukufu ya Zanzibar, uhuru pamoja na muungano wetu.
Nchi yetu ni nchi ya amani na ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa asili Duniani hivyo ni dhahiri maadui hawawezi kukosekana.
Maadui wapo na wataendelea kuwepo watatafuta kila mbinu kutudhoofisha kwa maslahi yao,kwa sasa wameminywa kila kona na mzalendo Magufuli hivyo wameamua kutafuta kila njia kumtikisa lakini wamegundua kuwa Rais Magufuli ni mwamba imara usiotikisika.
Tuendelee kumuombea kheri Rais wetu bila kukhofu kelele za mabwanyenye au mawakala wao aliongeza Ndg. Ngozi
Ndg. Ngozi aliwashukuru wana CCM na wananchi wote wa Wilaya ya Kondoa kwa mapokezi makubwa na kujitoa kwao kujumuika katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment