Monday, February 4, 2019

CCM DODOMA MJINI YAADHIMISHA MIAKA 42 KUZALIWA CCM.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Dodoma mjini leo tar 04/02/2019 kimefanya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kiwilaya kwa kuanzia ktk kata ya Nkuhungu

Ktk maadhimisho haya shughuli mbalimbali za kijamii zimefanyika hususan usafi ktk eneo la shule ya msingi Nkuhungu ktk kata ya Nkuhungu, kupanda miti ktk ofisi ya CCM kata ya Nkuhungu pamoja na kushiriki ujenzi wa vitega uchumi vya Chama Cha Mapinduzi kata ya Nkuhungu.

Pia maadhimisho haya yalifuatiwa na mdahalo mkubwa uliohusu uhai wa CCM na madhumuni ya kuundwa kwakwe viongozi mbalimbali walitoa mada juu ya uhai wa CCM tulipotoka, tulipo na tuendapo.

Maadhimisho haya yalikuwa sanjari na zoezi la usajili wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika mfumo mpya wa kielectronic vijana zaidi ya 200 walisajiliwa.

Mwenyekiti wa CCM ndg Robert Mwinje Amesema maadhimisho haya yataendea ktk tarafa zote 4 za Wilaya ya Dodoma mjini.

No comments:

Post a Comment