Tuesday, January 29, 2019

NAIBU WAZIRI MAVUNDE ASEMA SERIKALI KULASAHANI MOJA NA WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA AJIRA

Serikali inatarajia kuanza kutekeleza sheria ya adhabu ya papo kwa papo**(Compounding of offences)** kwa waajiri wote wanaokiuka masharti yaliyoanishwa katika *Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004* na *Sheria ya Taasisi za Kazi Na.7/2004* kwa kutoza faini kwa makosa yanayohusiana na masuala ya kazi ikiwemo suala la kutotoa mikataba ya kazi kwa waajiriwa.

Hayo yamesemwa leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni wakati Mh Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde*,kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu,akijibu swali la *Mh Munira Mustapha Khatibu(Mbunge Viti Maalum)* aliyetaka kujua kauli ya serikali juu waajiri ambao wanawakandamiza wafanyakazi wao katika kutoa mikataba.

Mavunde amewataka waajiri wote nchini kuzingatia matakwa ya sheria ya kazi na kwamba muda sio mrefu sheria ya kutoza faini papo kwa papo kwa makosa ya kazi itaanza kutekelezwa ili kuimarisha uwajibikaji upande wa waajiri,na pia kuwaasa wafanyakazi kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment