Serikali ya awamu ya Tano chini ya *Mh Rais Dr.John Pombe Magufuli* imeweka mipango madhubuti ya kuboresha huduma na mazingira katika makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu likiwemo kubwa la uwezeshwaji kiuchumi kupitia asilimia *2%* ya mapato ya ndani ya Halmashauri na Manispaa nchini.
Hayo yamesemwa jana katika Hotel ya Hyatt Regency na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde* kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu *Mh Kassim Majaliwa Majaliwa **wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya* *HAJI MANARA FOUNDATION** ambapo Mavunde alitumia nafasi hiyo kuelezea mipango Serikali katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa katika masuala ya siasa,kijamii na ushiriki katika ustawi na ujenzi wa Taifa Tanzania.
Mavunde alichukua fursa hiyo kumpongeza sana Mwanzilishi wa Taasisi hiyo *Ndg Haji Manara* kwa uamuzi na utayari kusaidia watu wenye mahitaji na kuahidi kwamba Serikali itatoa kila ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika kutimiza majukumu yake hasa katika kutoa elimu kwa jamii juu ya nafasi ya watu wenye ulemavu katika Jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo,**Ndg Haji Manara** ambaye pia jana alizindua perfume yake iendayo kwa jina la *De La Boss*,amesema Taasisi hiyo ni itasaidia kuwajengea uwezo watu wenye Ualbino pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuepukana na dhana potofu juu ya watu wenye ualbino,ambapo pia alibainisha kwamba
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,**Mh Paul Makonda **ametumia nafasi hiyo kumpongeza Haji Manara kwa ubunifu mkubwa na kuitaka jamii kuwaunga mkono watu wanaoleta mabadiliko na fikra mpya na sio kuwavunja moyo kwa majungu na maneno yasiyofaa.
No comments:
Post a Comment