Thursday, January 24, 2019

MWENYEKITI UVCCM TAIFA CMD KHERI JAMES (MCC) AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA ASASI ZA KIRAIA TANZANIA

Dar es Salaam

*Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Kheri James amezungumza na Viongozi mbali mbali wa Asasi za Kiraia wakati akifungua Kongamano hilo leo katika ukumbi wa Karimjee.*

Akizungumza katika kongamano hilo Ndg Kheri denis James amezipongeza asasi mbali mbali za Vijana kwa Kuendelea kuwa msaada wa masuala mbali mbali katika jamii na Tanzania kwa ujumla

“Leo tumeitana hapa kama Vijana kwanza Kufahamiana pamoja na kujadili Fursa mbali mbali kwa pamoja ili kupata namna bora ya kuzitatua changamoto mbali mbali zinazo wakabili Vijana”Alisema Comered kheri wakati akifungua Kongamano hilo

Pamoja na mambo mengine Comred kheri James ametumia fursa hiyo kuitaka serikali kuboresha na kupunguza gharama mbalimbali katika Vyuo mbalimbali vya ufundi ili kutoa fursa kubwa kwa Vijana wengi kuendelea kujifunza fani mbali mbali ili kujiajiri na kutoa mchango Katika jamii kuliko kutegemea kuajiliwa  na kusisitiza ya kuwa Tatizo la Ajira kwa Vijana duniani ni changamoto hivyo lazima Serikali iangalie namna bora ya Kuwekeza zaidi katika vyuo vya ufundi

Pia Ndg Mwenyekiti aliendelea kuwasisitiza Viongozi hao kuchukua hatua katika taasisi zao kuzuia changamoto  za kimaadili pamoja na kuwaunga Mkono Viongozi  walioaminiwa katika maeneo mbali mbali nchini kote. “Jukumu la kuwatia moyo Vijana walioaminiwa tunalo sisi ,Vijana tusiwe watu wa kuwahukumu Vijana wenzetu tunatakiwa kuwaombea kwa sababu kijana kupewa Nafasi ni jambo muhimu twendeni tukawasaidie kutimiza wajibu wao ili tuendelee kulijenga taifa letu”.

Aidha amewataka Viongozi hao kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika juhudi mbali mbali anazozifanya kuhakikisha anatekeleza Ilani ya CCM 2015-2020. Alisema “Rais magufuli Ana imani kubwa na Vijana wa Tanzania,Tanzania ya Viwanda mnufaika mkubwa ni kijana, miundombinu ya kisasa inajengwa kwa ajili ya Vijana,hivyo tunalojukumu la kumlinda Rais wetu Kama vijana wa Taifa hili. Kwa kipindi chake hiki cha miaka 3 amefanya mambo makubwa sana sana hivyo lazima kama vijana tumlinde kwa pamoja.

*#kulindaNaKujengaUjamaa*
*TukutaneKazini*

No comments:

Post a Comment