Monday, January 21, 2019

KATIBU MWENEZI SIASA NA ITIKADI CCM TAIFA COMRADE POLEPOLE AMEFUNGUA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO UVCCM SENETI VYUO VIKUU MKOA DODOMA

Image result for POLEPOLE
Katibu wa itikadi na Uenezi CCM Ndg Humphrey Polepole leo amefungua Semina ya kuwajengea uwezo Wanachama na Viongozi wa Uvccm Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma .
Ndg Humphrey polepole pamoja na mambo mengine amewataka wasomi hao kuendelea kujitahidi sana katika masomo yao na kufikiri katika suala la kujiajiri
“Ujana ni wakati na wakati kamwe haurudi nyuma ,tufahamu siri pekee ya kufanikiwa kwa mtu yeyote inategemea namna anavyotazama na kuthamini mambo Ni mtazamo chanya pekee ndiyo humvusha mtu katika mafanikio hivyo ipo haja ya sasa kujikita katika kutazama fursa zinazowazunguka na kuongeza ubunifu katika kujiajiri zaid “
Aidha Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana Mwl Raymond Mwangwala amewataka wasomi hao kutumia usomi wao katika kuisaidia jamii inayo wazunguka pamoja na kutumia elimu zao kukisaidia chama cha mapinduzi katika nyanja mbali mbali.
Akitoa Shukrani kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Khamana Juma Simba ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali za Elimu
na kuwataka Wanachama hao kuwa mabalozi wazuri wa kuisemea Serikali hiyo.
Aidha ndg Kamana ameendelea kuwahakikishia Wanachama hao kwa usimamizi mzuri wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Comred Kheri Denis James idara itaendelea kusimamia na kutoa mafunzo mbalimbali nchi nzima kwa makada wote wa Seneti za Vyuo vikuu ili kuwajengea uwezo wa kifkra juu ya Kuzifahamu fursa mbali mbali za wasomi hao kujiajiri kabla ya kusubiri kuajiliwa
Katika mafunzo hayo mada mbali mbali zilizo wasilishwa ni:
*1:Fursa katika Kujiajiri* iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa.
*2:Athari na faida za matumizi ya mitandao ya kijamii* iliyowasilishwa na Comred Kaiza
*3:Uzalendo:* iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
*4:Nguvu ya Mwanamke katika uongozi* iliyowasilishwa na Wabunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na Vijana Mhe Zainabu Katimba pamoja na Mhe Mariam Ditopile.
Pia katika mafunzo hayo yaliudhuliwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM anaetokana na UVCCM Comred Mussa Mwakitinya,Mwenyekt wa Uvccm Mkoa wa Singida Dkt Denis Nyiraha,Mjumbe wa Baraza kuu la Uvccm Dickson Mazanda,Mbunge wa Viti Maalum anaetokana na Vijana Mhe Munira Khatibu pamoja na katibu wa CCM Wilaya Dodoma Mjini Ndg Gress Shindika.
*#TukutaneKazini

No comments:

Post a Comment