Sunday, December 2, 2018

UVCCM MKOA DODOMA YAWASHUKURU VIJANA

Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU leo tumetimiza mwaka m'oja tangu mimi BILLY CHIDABWA kuwa mwenyekiti wa vijana Mkoa wa Dodoma.

Pia nawashukuru sana vijana wenzangu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuendelea kuniamini na kunipa kila aina ya ushirikiano pamoja na ushauri nasema asanteni sana, naamini ktk miaka yangu minne iliyobaki yapo mengine mengi makubwa mimi na wenzangu tumepanga kuyafanya na hakika ni mema kwa mustakbari wa jumuia yetu, chama chetu pamoja na jamii iliyotuzunguka.

Pia shukran zangu za pekee ziwaendee viongozi wenzangu wa CHAMA CHA MAPINDUZI kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa kuendelea kunipa ushirikiano hususan inapobidi ushauri ktk kipindi chote cha mwaka wangu m'oja.

Hakika ninawashukuru sana kama ipo sehemu mimi kama mwanaadam sijakamilika, niliwakwaza kwa kujua ama kwa kutokujua basi Ni naomba radhi na hakika ktk muda uliobaki unatosha kujirekebisha kwa kuwa nimejifunza mengi.

Mwisho kabisa nimshukuru mheshimiwa mwenyekiti CCM Taifa NDG JOHN POMBE MAGUFULI kwa imani kubwa aliyoendelea kuonesha kwetu sisi vijana na hakika mimi kama kiongozi mkuu wa vijana ktk Mkoa wa Dodoma, naamuahidi sitoiangusha imani kubwa uliyonayo kwetu vijana ktk mukitumikia chama na Taifa kwa ujumla.

Hakika tuna kila sababu ya kukuunga mkono kwa namna ambavyo ulivyojitoa kwa ajili ya Watanzania wanyonge wa nchi hii.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitokushukuru Rais Magufuli kwa yote uliyotufanyia na unayoendelea kutufanyia wana Dodoma hususan kwenye miundo mbinu, huduma za maji, huduma za afya kubwa zaidi kutekeleza ahadi yako ya kuyahamishia rasmi makao makuu ya chama na serikali kwa vitendo ktk jiji la Dodoma tunasema asante sana na tunakuahidi kuzidi kuwa sauti yako.

VIVA VIJANA VIVA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
VIJANA TUNA KESHO NYINGI
TUKUTANE KAZINI.

No comments:

Post a Comment