Tuesday, December 4, 2018

KATIBU MKUU CCM DR BASHIRU ALLY AFUNGUA SEMINA YA JUMUIA ZA CCM TANZANIA.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili Dodoma, Dkt Bashiru amepongeza watendaji hao kwa kuendelea kukitumikia chama hicho kwa kila mmoja katika nafasi yake.

Dkt Bashiru Ally Kakurwa amewaeleza watendaji hao juu ya kuimarika kwa chama cha Mapinduzi pamoja na kusifia utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020.

amesema"Chama Chetu kinaendelea kuimarika na kuisimamia Serikali, kwa hii miaka mitatu ya utekelezaji wa ilani ya CCM tumepata mafanikio makubwa sana sana.Mafanikio haya yanatokana na uongozi bora wa CCM chini ya Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama Chetu Dkt John Pombe Magufuli"

Ndg Katibu Mkuu ameelezea umuhimu wa mafunzo na kusema kwamba mafunzo hayo ni moja ya nyenzo ya kuwajengea uwezo na maarifa watendaji na viongozi wa CCM.

Pia katibu Mkuu ameelezea Vipaumbele vya Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake kuwa ni pamoja na

1. Kuzifufua shule zote zinazomilikiwa na Umoja wa Wazazi
2. Kufufua vyuo vya chama vya itikadi na uongozi zoezi litakalosimamiwa kwa ukaribu zaidi na UVCCM
3. Chama kuendelea kusimamia Umoja wa Vijana ili jumuiya hiyo iendelee kuwa kitovu cha kuandaa vijana kuanzia ngazi ya chipukizi
4.Jumuiya ya vijana kuzunguka nchi nzima na kurejesha vikundi vya Hamasa ikiwa ni pamoja na kuwasimamia wasanii walio ndani ya chama cha mapinduzi kutumia sanaa katika kutangaza kazi zinazofanywa na CCM pamoja na serikali
5. Jumuiya zote lazima ziendelee na ziwe mstari wa mbele katika kumuunga mkono na kuunga mkono kazi zote zinazofanywa na serikali ya tano chini ya Rais Dr. Magufuli
6. Umuhimu wa kutii katiba ya CCM
7. Kuendelea kujenga imani ya itikadi ya Ujamaa kwa wananchama wake na wananchi wote kwa ujumla

Vile vile Dr. Bashiru amesisitiza na kusema katika uongozi wa sasa wa CCM hakuna tena nafasi ya kuunda timu za urais na kwamba yote yanayofanywa kwa sasa na CCM yana msingi wa kikatiba.

*Semina hiyo itakuwa ya siku mbili, tarehe 4/12 mpaka tarehe 5/12 Dodoma.*

Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipikizi UVCCM

No comments:

Post a Comment