Tuesday, November 27, 2018

ZIARA YA KATIBU MKUU CCM

Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally Kakurwa, leo hii amewasili na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali Mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Katika ziara yake Ndg Katibu Mkuu atazungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mkoa pamoja na wajumbe wa kamati za siasa za Wilaya zote za Mkoa wa Iringa katika mkutano utakao fanyika katika ukumbi wa siasa ni kilimo.

Mara baada ya mkutano huo Dkt Bashiru Ally atatembelea na kukagua eneo lote la Chuo Cha mafunzo Ihemi ikiwa ni maandalizi ya kukifufua chuo hicho ili kuwa kituo cha mafunzo ya kufundishia viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment