Sunday, November 25, 2018

MKOA WA MARA WAMUUNGA MKONO RAIS KWA VITENDO

UVCCM Mara yamuunga mkono Rais Magufuli kwa vitendo.

Umoja wa vijana mkoa wa Mara umezindua bidhaa zake za ujasiri amali ikiwa ni juhudi za kuelekea kuwa na viwanda vidogovidogo kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa vijana mkoani Mara.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika Leo kwenye ukumbi wa CMG Motel Tarime mwenyekiti wa UVCCM Mara Jacobo Mangaraya alisema lazima vijana wawe wa kwanza kuendana na kasi ya Rais kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati.

"Leo tumetaka tuwaoneshe ninitunafanya na tunataka kufika wapi,lzm tuwe na vijana wanaomiliki uchumi ili wafanye siasa bila njaa,lzm tupambane kwenda na kasi ya Mh Rais Tanzania tufikie uchumi wa kati,ndio maana Mara tumeanza" Alisema Mangaraya

Aidha alisema ndani ya uongozi wake anatarajia kila wilaya UVCCM imiliki mradi ili vijana waweze kupata ajira na kukuza kipato cha jumuiya pamoja na vijana kwa ujumla.
Katika uzinduzi huo bidhaa mbalimbali zilizinduliwa ikiwemo mradi wa maziwa,sabuni aina zote na ushonaji.

No comments:

Post a Comment