MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabir Shekimweri amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya ulimajj wa zao la korosho ili kuimarisha uchumi wa wilaya hiyo na kuenzi kauli ya Rais ya Tanzania ya viwanda.
Shekimweli ametoa kauli hiyo hii Leo alipo kuwa akizindua Mpango mkakati wa wilaya wa kuimirisha uchumi wa wilaya hiyo na ulimaji wa zao la korosho ambalo ni zao la kimkakati Katika kukuza uchumi wa wilaya .
Amesema” Rais Kama ametangaza Tanzania ya viwanda lazima tuanze kujipanga Katika kuanza kuzalisha malighafi za kuendesha viwanda hivyo”amesema.
Aidha Shekimweli amesema ni lazima vijiji vyote vilivyoko kwenye maneo ambayo udongo wake unastawi zao la korosho kuwa na shamba darasa la kijiji la Mfano kwa zao hilo.
Pia amewaagiza maafisa Kilimo wa Kata kuhakikisha wanawasaidia wakulima kwa kuwapa maelekezo ya kitaalamu Katika upandaji na usimamizi wa zao hilo ili liwe na tija kwa wakulima hao.
Shekimweri amesema Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 aliiagiza kila kijiji kuwa na shamba darasa la korosho jambo alilosema bado halijatekelezwa Kwa vijiji vingi vya Mpwapwa.
Aidha Shekimweri amewaomba madiwani na viongozi wote wa kuteuliwa na kuchaguliwa kuweza kuhimiza jamii juu ya mabadiliko ya Mpwapwa mpya inayolenga Katika mabadiliko ya kiuchumi,Uadilifu,uwajibikaji,ufanisi,ubunifu na mafunzo, kuwajali wateja na moyo wa kufanya kazi .
Hata hivyo amesema zao la korosho limefanyiwa utafiti na kubaini kuwa kwa kuwa na zao mkakati la wilaya linalo lenga kuinua uchumi Pamoja na uboreshaji wa huduma za jamii ikiwemo Elimu, afya Pamoja na huduma za maji.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe, George Fuime amesema kama zao la korosho likaitikiwa kwa mwamko chanya na jamii basi ndani ya miaka mitano ijayo Mpwapwa itaimarika kiuchumi na kimazingira.
Amesema wananchi lazima wafuate maelekezo ya wataalamu ili kuweza kupata tija katika zao hilo.
Pia amewataka wananchi kuweza kuzingatia taarifa za hali ya hewa ili kuweza kuandaa mashamba yao kwa msimu wa kilimo kwa mwaka 2018/2019.
Mmoja wa wananchi ambao ni wakulima wa korosho bwana Yusuph Mwawole ambae amelima hekali 20 za za korosho amesema kiangazi na upatikaji wa dawa za kupiga katika zao hilo kunatishia uzalishaji kupungua lakin pia baadhi ya miche kunyauka.
Kauli mbinu ya Mpango mkakati huo ilikuwa ni INUKA TUIJENGE MPWAPWA MPYA korosho ni dhahabu ya Kijani.
No comments:
Post a Comment