Saturday, December 8, 2018

MAVUNDE AZINDUA TAASISI YA WASANII DODOMA KWANZA.

**MBUNGE MAVUNDE AZINDUA TAASISI YA WASANII DODOMA,AKABIDHI OFISI NA STUDIO*

Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* leo amezindua rasmi Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma.Uzinduzi huo umefanyika leo katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road,Dodoma kwa kujumuisha wasanii wa ndani na nje ya Dodoma.Ofisi hizo na studio
Zitatumiwa  na Wasanii wote kupitia umoja wa na Vilabu vya wasanii.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge Mavunde amewataka wasanii wa Dodoma kuwa na *UPENDO*,**MSHIKAMANO** na *UMOJA* ili kuweza kufikia mafanikio na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafika mafanikio ya juu katika sanaa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini *Mh Patrobas Katambi* amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna anavyowatumikia wanaDODOMA na kuahidi kushirikiana nae kuwasaidia Vijana wasanii ili wapige hatua zaidi katika mafanikio ya kwenye sanaa.

No comments:

Post a Comment