Tuesday, December 11, 2018

UVCCM MKOA WA DODOMA WAMPONGEZA RAIS

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma ndg Billy Chidabwa amemshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya vijana wote Mkoa wa Dodoma kwa kuonesha kwa vitendo kuwajali wafanya biashara wadodogo wadogo(Machinga)

Kwa kuwawekea mfumo rasmi wa vitambulisho utakaopelekea kutambulika ktk jamii pia kuondoa kero ya kamata kamata iliyokuwa ikipelekea usumbufu kwa kada hii ya wafanyabiashara.

Pia amempongeza kwa kutolea tamko la mamlaka za mapato Tanzania TRA na ZRA kuweka kodi rafiki.

Pia wamempongeza Rais kwa tamko la kuitaka TPA na TRA kuondoa urasimu ktk bandari zetu kunakopelekea mizigo kukaa kwa muda mrefu bandarini kunakopelekea kuwakatisha tamaa wawekezaji.

Asante sana Rais Magufuli tunaahidi kukuunga mkono ktk kila jema kwa nchi hii.

No comments:

Post a Comment