Leo Naibu Waziri ndg Nyongo amezindua rasmi ugawaji wa pembejeo za kilimo na mbegu kwa vijana 3500 wa Mkoa wa Dodoma.
Zoezi hili limefanyika ktk viwanja vya Nyerere square Mkoani Dodoma.
Ndg Nyongo amewaasa wote watakopewa hizi mbegu na pembejeo wazitumie kwa tija iliyokusudiwa
Nae Naibu spika Dr Tulia Acson amemshukuru sana Mbunge Ditopile kwa juhudi zake anazoendelea kuzifanya ndani ya chama na kwa jamii kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kumshukuru kwa tukio lake la kugawa vifaa vya ofisi ktk ofisi zote za chama Mkoa wa Dodoma.
Mbunge wa Mtera ndg Livingston Lusinde hakusita kumpongeza mbunge Ditopile kwa kuwa mbunge wa kwanza wa viti maalum Mkoa wa Dodoma kufanya jambo kubwa kama hili.
Nae mwakilishi kutoka Wizara ya kilimo ndg Silvesta Kashaiga amewahakikishia wana Dodoma uhakika wa wataalamu pamoja na soko la alizeti watakayoilima, pia zipo fursa nyingi kutoka kwa wafadhili mbalimbali ameahidi kuwashirikisha ili wawe sehemu ya wanufaika wa ufadhili huo.
Nae mbunge ambae ndiye mratibu wa zoezi hili ndg Ditopile amewaasa kuzitumia vizuri hizi pembejeo pamoja na mbegu ili ziweze kuleta tija iliyokusudia pia ameahidi kuwa zoezi hili kuanzia sasa ni endelevu.
Pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kutupendelea wana Dodoma pia naushukuru uongozi wangu wa CCM Mkoa wa Dodoma na jumuia zake.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya vijana wote amemshukuru sana mbunge Ditopile kwa hili na mengine yote aliyokwishayafanya.
No comments:
Post a Comment