Leo uongozi wa vijana Mkoa wa Dodoma umeendesha uchaguzi wa chipukizi ngazi ya Mkoa na kufanikiwa kupata viongozi wake.
Mgeni rasmi ktk uchaguzi huo mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma ndg Billy Francis Chidabwa amewaasa chipukizi walioteuliwa ktk ngazi ya Mkoa kurudisha juhudi ktk masomo yao ili kuondoa dhana kwa baadhi ya wazazi kuwa mtoto kuingia ktk chipukizi kubapunguza uwezo wake masomoni.
Amesisitiza kuwa kioo kwa watoto wenzao ili kukiletea heshima chama chetu cha mapinduzi kwakuwa chipukizi ni UVCCM wa baadae na UVCCM ni viongozi wa chama wa baadae.
Hivyo ni muhimu kuishi kwa nidhamu ktk kipindi chote cha uongozi na nje ya uongozi.
Niwasihi tumuunge mkono mheshimiwa Rais wetu ameonesha kuwajali chipukizi kwa kutoa elimu bila malipo hii yote ni ishara ya UPENDO wake kwenu.
Nikupongeze mwenyekiti mwenzangu wa Mkoa kupitia idara ya chipukizi mdogo wangu Luoga kwa ushindi mkubwa ulioupata wewe na viongozi wenzio wote.
No comments:
Post a Comment