Vijana UVCCM Mkoa Dodoma tunaendelea kuipongeza serikali yetu na Rais wetu Dr John Joseph Pombe Magufuli kwani amezidi kuutafuna mfupa ulioshindikana kwa muda mrefu.
Tumeendelea kuwa na umeme usiovutia wawekezaji wa viwanda pia tumeendelea kuwa na shirika la ndege tegemezi kwa muda mrefu, lakini Rais Dr Magufuli amesema tumechezewa kwa muda mrefu ila sasa basi.
Leo tunapokea ndege nyingine kubwa aina ya Air bus A220-300 ni fahari kwa Tanzania fahari kwa serikali inayoongozwa na CCM Tanzania.
Ifikie kipindi serikali inayoongozwa na CCM ihukumiwe kwa tuliloliahidi kwa kuangalia lipi imetekeleza na lipi haijatekeleza ili tutende haki kwa watoa ahadi.
No comments:
Post a Comment