Thursday, December 6, 2018

MBUNGE MAVUNDE ATIMIZA METHALI

Leo mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ndg Peter Mavunde ametimiza ile methali isemayo rafiki wa kufa na kuzika.

Ametimiza methali hii kwa kutimiza moja ya ahadi alizozitoa ktk jimbo la Dodoma mjini.

Mbunge Mavunde leo amekabidhi gari hilo la kubebea maiti kwa mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya wakazi wa jimbo la Dodoma mjini.

Ktk makabidhiano haya mgeni rasmi alikuwa RC Dr Benelith Mahenge pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali ya Wilaya na Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na dada yetu mjumbe wa kamati kuu CCM Leyla Burhani Ngozi ambae pia ndiye mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, mwenyekiti CCM Mkoa wa Dodoma ndg Mkanwa, katibu CCM Mkoa wa Dodoma ndg Jamila Yusuf, mwenezi Mkoa Dodoma ndg Msunga(Mwenge), viongozi wa baraza la wazee, Mwenyekiti Uvccm Mkoa wa Dodoma, katibu Uvccm Mkoa ndg Asia Halamga na wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa, pia imehudhuriwa na mwenyekiti CCM Wilaya Dodoma ndg Robert Mwinje, katibu CCM Wilaya Dodoma mjini ndg Pili Mbanga, mwenyekiti UVCCM Wilaya ndg Said Kasote, mwenyekiti UWT Dodoma mjini, katibu UVCCM ndg Ahmad Kibamba na wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya Dodoma mjini. Na viongozi mbalimbali wa chama na serikali na wana Dodoma. Viongozi wa taraka mbalimbali wakiongozwa na ndg Remedius Emanuel pamoja na ndg Semindu, viongozi wa Dini mbalimbali, waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na vikundi mbalimbali vya sanaa.

Mavunde amesema hili gari gharama zote zametengenezo pamoja na Dereva vitakuwa ni gharama zake, pia amewashukuru wadau mbalimbali akiwepo Haleluya Kessy, Karim Bhanji na Ndg Mwinuka wa Njombe garage kwa kutoa Lita 50 za mafuta kwa kila mwezi kwa ajili ya uendeshaji wa hili gari, pia nawashukuru sana viongozi wote wa CCM Mkoa na Wilaya pia nawashukuru wabunge wote wa viti maalum ndg Mariam Ditopile, Ndg Bura na bi Fatma Toufiq kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa ktk yote ninayoyafanya.

No comments:

Post a Comment