UVCCM MKOA WA DODOMA YATOA TAMKO.
Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Dodoma ndg BILLY CHIDABWA kwa niaba ya kamati ya utekelezaji UVCCM Mkoa wa Dodoma ikiambatana na mbunge anayewakilisha vijana Mkoa wa Dodoma ndg Mariam Ditopile leo tarehe 22/11/2018 imetoa tamko la shukran kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kwa maamuzi yake sahihi kwa wakati sahihi juu ya kufuta sherehe za 9 Dec 2018 na badala yake pesa zote zaidi ya tsh's 995milioni kuzielekeza ktk ujenzi wa hospitali kubwa yenye hadhi ya makao makuu ya nchi ktk Wilaya ya Dodoma mjini ndani ya kata ya Ihumwa Mkoani Dodoma.
Kwa pamoja tunasema asante sana Mh Rais kwa maamuzi yako ya kizalendo, kishujaa na yanayolenga kuwanufaisha wanyonge na wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na viunga vyake.
Tunaamini kabisa ujenzi wa hospitali hii utasaidia sana kuondoa tatizo la mlundikano wa wagombea ktk hospitali zingine na zaidi kusaidia tatizo la ukosefu wa huduma nzuri za mama na mtoto ktk maeneo haya.
Sisi vijana kama nguzo ya maendeleo ya jamii na Taifa, tumeazimia kwa pamoja, mvua inyeshe, jua liwake kwa gharama yeyote tutashirikiana na serikali yetu ya Wilaya, Mkoa na Taifa kuhakikisha kuwa hospitali hii kubwa na ya kisasa inakamilika kwa wakati na ufanisi mkubwa.
Vijana tupo tayari kuanzia sasa kufanya kazi zote za nguvu kazi, kitaalamu na kujituma kwa hali na mali kuhakikisha hospitali hii inakamilika haraka iwezekanavyo.
Kwa kuunga mkono dhamira ya kweli na ya dhati ya Mh Rais wetu.
Vijana wote tumeazimia kushiriki ktk kufanya usafi ktk hospitali zetu zote za Mkoa wa Dodoma pamoja na kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Zoezi hili litafanyika tarehe 09/12/2018 kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru lakini pia kuunga mkono kuhisi za comrade Magufuli ktk kuboresha sekta ya Afya hapa Tanzania.
Pia tunamshukuru Mh Rais kwa mengi aliyokwishayafanya Mkoani kwetu hususan ktk ujenzi wa SOKO LA KISASA(CENTRAL MARKET) Ujenzi na ukarabati wa mtandao wa BARABARA YA KISASA inayounganisha mji wa Dodoma na Mikoa jirani pamoja na barabara za ndani, Ujenzi wa KITUO CHA KISASA CHA MABASI ya mikoani na nchi jirani(EAST AFRICA) Ujenzi wa RELI MPYA na ya kisasa, ujenzi wa KIWANJA KIKUBWA CHA NDEGE na Mi radi mbalimbali ya maji safi na maji taka.
Vijana tunasema
HAPA KAZI TU! MPAKA HOSPITALI YA UHURU IKAMILIKE.
MUNGU M'BARIKI RAIS WETU MAGUFULI,
MUNGU WABARIKI VIJANA,
MUNGU UBARIKI MKOA WA DODOMA,
MUNGU IBARIKI HOSPITALI YA UHURU,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
TUKUTANE KAZINI.
No comments:
Post a Comment