Wednesday, January 23, 2019

MBUNGE MAVUNDE ATIMIZA AHADI YAKE KWA MTOTO ALIYEKATWA MIGUU YOTE DODOMA.

*MBUNGE MAVUNDE ATIMIZA AHADI YAKE KWA MTOTO CHRISTOPHER MASAKA,AIOMBA JAMII KUSAIDIA WENYE MAHITAJI*
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony P. Mavunde * ameiomba jamii kuwasaidia watu wenye mahitaji ili kuwawezesha kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mavunde ameyasema hayo leo katika Shule ya *Fountain Gate Academy* wakati akimkabidhi mtoto Christopher Masaka kwa Uongozi wa shule hiyo na kusajiliwa rasmi kama Mwanafunzi wa shule hiyo.
Mtoto Christopher Masaka alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa viungo uliopelekea kukatwa miguu yake yote miwili katika *Hospital ya Benjamin Mkapa* ambapo Hospital ya Benjamin Mkapa ilitoa msaada wa kiti mwendo *“wheelchair”* kwa mtoto huyo na Mbunge Mavunde kumpatia Miguu ya bandia na kumuahidi kumsomesha katika shule za Jijini Dodoma.
Akizungumza kwa furaha kubwa,Mtoto Christopher ameshukuru Mbunge Mavunde kwa kumsaidia kufika hapo alipofika na kuahidi kusoma kwa bidii na kujituma.
Naye Mkurugenzi wa Shule za Fountain Gate Academy *Ndg Japhet Makau * amesema wamempokea Mtoto Christopher na atasoma bure kwa muda wote kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Mbunge Mavunde katika shule yao ambayo mpaka sasa inasomesha zaidi ya watoto yatima 20 kwa ufadhili wa shule.

No comments:

Post a Comment